Discuss & Debate | Share | Learn

www.ask.or.tz

Our Partners
#19022
Image

Maoni ya watu kuhusu utumwa ni kwamba umetupwa kwenye mapipa ya takataka ya historia, wakati bado athari za ushenzi huu wa kuchukiza ambao mwanzo wake ulikuwa dhidi ya Waafrika, unajitokeza wenyewe kwa sura mpya na mbaya zaidi kwenye karne ya 21. Tangu kupigwa marufuku kwake rasmi katika mwaka wa 1863, utumwa umechukuwa sura ya uovu na ya kuchukiza zaidi, katika muundo wa utumwa uliopakazwa mafuta kwa mgongo wa chupa. Utandawazi kupitia umiliki wa nguvu za kuzalisha unaofanywa na “Muungano wa Kimataifa wa Wakiritimba” (Multi National Cartels) ni muundo mpya wa utumwa.

Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi anaelezea suala hili la biashara ya utumwa kwa muktadha wake halisi. Allamah Rizvi amekiandika kitabu hiki kwa uwezo mkubwa na jitihada. Kama ilivyo kwa msomi mtafiti kama yeye, ameshuhgulikia mada ya kitabu hiki bila upendeleo, Ameupanga ukweli baada ya ukweli kutoka kwenye historia; amenukuu kutoka kwenye Qur’an, Hadithi na waandishi wa zama za leo kuhusu somo hili, na ameonyesha sheria za Kiislamu na zile zilizotumika kabla ya Uislam. Ameonyesha waziwazi kwamba ustaarabu wa Kimagharibi sio bingwa mkubwa kiasi hicho wa kuwaokoa watumwa kama unavyojionyesha na kujigamba. Kwa kweli kitabu hiki kitathibitisha kuwa kifungua macho kwa wale ambao hukubali bila kuchunguza kuhusu propaganda ya ubinadamu wa Kimagharibi.

Jina la Kitabu : Utumwa : Mtazamo wa Kiislamu na wa Nchi za Magharibi
Mwandishi : Sayyid Saeed Akhtar Rizvi
Mtafsiri : Salman Shou
Mchapishaji : Al-Itrah Foundation
ISBN : 9987902243

PDF: https://www.shia-maktab.info/index.php/ ... ad&fid=470

Imam Ja'far al-Sadiq (AS) was a great Islamic scho[…]

Aerobics

Get Ready to Move, Girls We are excited to announ[…]

Friday Vibes

Imam Ali (A.S.)‏ رُبَّمَا أُخِّرَتْ عَنْكَ ال[…]

YAWME GHAM

https://youtu.be/pwtF72taZWk?si=K-ypf7WlM5D09RgT […]

Ask4help Counseling Helpline