Discuss & Debate | Share | Learn

www.ask.or.tz

Our Partners
#18949
Image

Baada ya kufariki Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Masahaba walihitilafiana katika baadhi ya mambo; na kubwa kuliko yote lilikuwa kuhusu kiongozi wa Waislamu baada yake (s.a.w.w). Hili lilileta mzozo mkubwa sana ambao bado unafukuta mpaka sasa. Mzozo huu ulisababisha kutokea kwa makundi mawili makubwa: 1) Wanaounga mkono Makhalifa waliochaguliwa na Waislamu, na 2) wanaomuunga mkono Imam Ali bin Abu Talib (a.s.) kwa madai kwamba yeye aliteuliwa na Mtume mwenyewe kwa amri ya Mola kuwa mrithi wake. Kundi hili la pili lilijulikana kwa jina la Shia wa Ali. Matapo haya mawili yaliendelea kuwepo kwa muda yakijulikana kwa majina yao hayo. Baadae, kundi hili la kwanza (la Makhalifa) likagawanyika katika makundi mengi ya kifikihi, katika hayo manne ndio maarufu sana: Hanafi, Maliki, Shafii na Hanbali. Haya hayakutokea mara moja; kila moja lilitokea kwa wakati wake (ukisoma historia ya Uislamu utauona ukweli huu). Ama Mashia wao wamebakia na jina lao hilohilo mpaka leo (soma historia ya madhehebu za Kiislamu). Baada ya muda kupita, yakajitokeza matapo mengine kwa majina tofauti tofauti. Kwa mfano, Wahabi, Ansar Sunna, Salafia, n.k.

Mwandishi wa kitabu hiki anaelezea kuhusu tapo hili la Usalafi. Anaelezea kwa kina maana ya Usalafi (Salafiyyah), ulianzaje na lini, na athari yake kwa Waislamu. Tafadhali ungana naye ili upate kujua yaliyojiri katika historia ya Uislamu.

Jina la Kitabu : Historia, Maana na Lengo la Usalafi
Mwandishi : Sheikh Ja’far Subhani
Mtafsiri : Hemedi Lubumba
Mchapishaji : Al-Itrah Foundation
ISBN : 9789987170333

PDF: http://www.shia-maktab.info/index.php/e ... ad&fid=366

Imam Ja'far al-Sadiq (AS) was a great Islamic scho[…]

Aerobics

Get Ready to Move, Girls We are excited to announ[…]

Friday Vibes

Imam Ali (A.S.)‏ رُبَّمَا أُخِّرَتْ عَنْكَ ال[…]

YAWME GHAM

https://youtu.be/pwtF72taZWk?si=K-ypf7WlM5D09RgT […]

Ask4help Counseling Helpline