Discuss & Debate | Share | Learn

www.ask.or.tz

Our Partners
#18923
Image

Hii ni tafsiri ya Sura Al-Ahzaab pamoja na maelezo yake kwa lugha ya Kiswahili.

Mbali na kuzieleza kwa urefu aya mbalimbali zilizomo katika sura hii, Sheikh Abdilahi Nassir ameongeza vijalizo vinne, baada ya kumaliza tafsiri ya sura yenyewe.

Katika Kijalizo cha Kwanza amejadili suala la ahlul bayt ni nani. Kwa hujja za Qur'ani Tukufu na sunna za Mtume Muhammad (s.a.w.w.), alizozifafanua kwa uwazi sana, ameonyesha. kwamba ahlul bayt si wake wa Mtume (s.a.w.w.) wala si Banii Hashim (masharifu) wote, bali ni watu maalumu katika Nyumba ya Bwana Mtume (s.a.w.w.) walioteuliwa na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) na kuhifadhiwa na kufanya dhambi na makosa. Yote hayo ameyajadili kiilimu na kimantiki.

Katika Kijalizo cha Pili amejadili suala la kuwa Mtume Muhammad (s.a.w.w.) ni Mtume wa mwisho au la. Kwa kutoa hujja zake katika Qur'ani Tukufu, Hadith za Bwana Mtume (s.a.w.w.), na za baadhi ya maimamu wanaofuatwa na mashia, komangano la maswahaba watukufu, yaliyosemwa na wafasiri wa Qur'ani Tukufu wa madhihabi mbalimbali - tangu karne ya kwanza hadi hii ya kumi na nne - kwa ushahidi wa makamusi ya tafsiri ya Qur'ani na ya lugha ya Kiarabu, ya Waislamu na wasio Waislamu, amethubutisha kwa hujja zisizokanushika kuwa Muhammad (s.a.w.w.) ni Mtume wa Mwisho; hakuji tena Mtume mwengine baada yake. Pia amezidondoa hujja zote zilizotolewa katika uk 735- 739 wa tafsiri ya Qur'ani Tukufu ya Makadiani na kuzijibu moja baada ya moja, kiilimu na kimantiki.

Katika Kijalizo cha Tatu, ameeleza kwa urefu hikima ya Mwenyezi Mungu kumruhusu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) kuwa na wake zaidi ya wanne kwa wakati mmoja, tafauti na wanavyoruhusiwa Waislamu wote: ya kuwa na wake wanne tu, sio zaidi, kwa wakati mmoja. Pia ameeleza hikima ya kila moja ya ndoa hizo pamoja na kuzibatilisha zile tuhuma zinazotolewa dhidi ya Bwana Mtume (s.a.w.w.) kwa kuowa wake wengi.

Katika Kijalizo cha Nne amethubutisha, kinyume na imani iliyoenea kwa Waislamu wengi, kwamba Mtume Muhammad (s.a.w.w.) - kama ilivyo kwa Waislamu wote - anarithiwa; na kwamba khatua iliyochukuliwa ya kumnyima binti yake (Bibi Fatma) urathi wake ni kinyume kabisa na Qur'ani Tukufu na Hadith mutawatir za Mtume Wake (s.a.w.w.).

Hiki ni kitabu cha kila Mwislamu kuwa nacho.

Jina la Kitabu : Sura al-Ahzaab : Tafsiri na Maelezo
Mwandishi : Sheikh Abdilahi Nassir
Mchapishaji : Ahlul Bayt Centre
ISBN :

PDF :
http://www.shia-maktab.info/index.php/e ... ad&fid=348

Imam Ja'far al-Sadiq (AS) was a great Islamic scho[…]

Aerobics

Get Ready to Move, Girls We are excited to announ[…]

Friday Vibes

Imam Ali (A.S.)‏ رُبَّمَا أُخِّرَتْ عَنْكَ ال[…]

YAWME GHAM

https://youtu.be/pwtF72taZWk?si=K-ypf7WlM5D09RgT […]

Ask4help Counseling Helpline