Bisamillahirahmanirahim. Amesema Mwenye utukufu wote: "Amtegemea Mwenyezi Mungu, yeye humtosheleza".
Ni kweli kwamba tunapata mafunzo mengi kutoka kwa maulamaa wote ikiwa sawa na kwamba walijitoa nafsi zao na mali zao katika njia ya Allah (swt). Uislamu umeharamisha kuomba na kuwategemea wengine badala ya Mwenyezi Mungu (swt) na umehimiza kwamba tujitole kwa ajili ya dini ya Allah (swt) na ndipo akasema Mwenye utukufu wote: "Watoke kundi miongoni mwenu wakatafute elimu..." (Qura'ni takatifu) na akasema Bwana Mtume (saaw)," Tafuteni elimu hata mukibidi kwenda china" na katika hadithi nyengine akasema Mtume (saaw)," Wino la watafutaji elimu ni bora kuliko damu ya mashahidi"-midad ulamaa afdal min dimaa shuhadaa". Na ndipo kutafuta elimu kukawa Wajibulkifaya na pia katika wakati huohuo wawepo waislamu ambao wawasaidie hao wanaoshughulika na kutuafta elimu kimali na kwa uwezo wote kwa sababu wajib la kujitaftia elimu ya dini limeondoka kwa wengine. Lakini hii ndio hali ya waislamu wa sasa hasa waliopo kwetu ambao wanaishi kwa uongo, kudanganya, kutotimiza ahadi, uifsadi na mambo mengi mpaka ikawa hakuna hata mmoja ambae anakula rizki ya halali hivyo imekuwa shida kujitoa nafsi zao na mali zao katika njia ya Allah (swt) kisha wakabaki kumsibiria Mahdi mwahidiwa au Mtume Issa

waje walaze mapanga zao kwenye vichwa vyao.
Wassallamunalaikum